Kumetokea
shambulizi katika shule moja ya upili wakati wanafunzi wakiwa
wamekusanyika shuleni humo mjini Potiskum Kaskazini Mashariki mwa
Nigeria.
Duru zinasema kuwa wanafunzi 47 wameuawa katika
shambulizi hilo linalosemeklana kufanywa na mshambuliaji wa kujitoa
mhanga ambaye alikuwa amevalia sare za shule.
Shambulizi lilitokea
wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika wakati wa asubuhi. Mji wa
Potiskum ambapo shule hiyo ipo, umekuwa kitovu cha mashambulizi ambayo
yamekuwa yakifanywa na Boko Haram.
Shule hiyo ni ya mafunzo ya
sayansi. Mwalimu mmoja alinukuliwa akisema kuwa alisikia mlio mkubwa wa
kutisha wakati bomu hilo lilipolipuka.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram huenda ndilo limefanya shambulizi hilo, ila taarifa bado hazijathibitisha hilo.
Kadhalika
kundi hilo limekuwa likishambulia shule katika harakati zake za miaka 5
likitaka kuunda dola ya kiisilamu huku likipinga elimu ya kimagharibi.
Wiki jana shambulizi la kujitoa mhanga lilifanyika mjini humo na kuwaua watu 15 wakati wa maandamano ya kidini.
No comments:
Post a Comment