Kituo kimoja cha televisheni nchini
Marekani kinachorusha kila siku kipindi cha mhubiri Pat Robertson
kiliomba radhi Jumatatu kwa madai yake potofu kwamba wasafiri
wanaokwenda Kenya wanaweza kupata maambukizi ya Ukimwi kwa njia ya
taulo.
"Dr Robertson alikosea kusema juu ya uwezekanao wa kupata
Ukimwi kwa njia ya mataulo," kimesema kituo cha Utangazaji cha Kikristo,
CBN, katika mtandao wa Facebook.
"CBN imegundua mara moja kosa
hili na kuondoa kauli hiyo kutoka kwa maktaba ya mtandao huo. CBN
inaomba radhi kwa mkanganyiko wowote."
Mhubiri huyo mwenye umri wa
miaka 84, mwinjilisti mkongwe ameonya katika kipindi chake cha "700
Club" cha Oktoba 16 kwamba wasafiri watalazimika kuchukua tahadhari ya
hali ya juu ya kiafya wawapo nchini Kenya.
"Unaweza kupata Ukimwi
nchini Kenya," Bwana Robertson aliwaambia watazamaji wake wanaokadiriwa
kufikia milioni moja. "Watu wana ukimwi. Unatakiwa kuwa makini. Nina
maana kuwa, mataulo yanaweza kuwa na virusi vya Ukimwi."
Madai ya Bwana Robertson haraka yalishambuliwa na makundi yanayojihusisha na masuala ya ugonjwa wa Ukimwi.
Wamesema
kuwa Ofisi ya serikali ya Marekani ya Masuala ya Afya ya kina Mama
inasema virusi vya Ukimwi haviwezi kuambukiza kwa njia ya "kushirikiana
vyombo vya chakula, mataulo na mashuka, simu au vyoo ."
'Hatari ya kutembelea Kenya'
Matamshi
ya Bwana Robertson yamekuja kutokana na swali alilotumiwa kwa njia ya
barua pepe na mtu asiyejulikana ambaye alielezea wasiwasi juu ya madhara
ya kutembelea Kenya wakati wa mlipuko wa Ebola barani Afrika.
Alimhakikishia
mtazamaji wa kipindi chake kuwa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini Kenya
akisema Kenya iko mbali na kitovu cha mlipuko wa Ebola, Afrika
Magharibi.
Lakini Bwana Robertson alieleza hatari ya kuambukizwa magonjwa mengine nchini Kenya pamoja na Ukimwi.
Mbu
wanaweza kusababisha madhara makubwa ya ugonjwa, amesema, akiongezea
kwamba, "usafi akielezea kuwa tatizo lingine. Unakunywa maji,
hayajachujwa, unaweza kupata ugonjwa wa matumbo"
No comments:
Post a Comment