Kama
sehemu ya vyanzo vyako vya habari ni mitandao kama vile website, blogs,
facebook, twitter na Instagram inawezekana hii stori ya Gwajima ambae ni
Muhubiri wa Injili kununua Helikopta uliiona hata zaidi ya mara
moja.Hata hivyo Muhubiri mwenzake Askofu Zacharia Kakobe Aug 10 2014
amenukuliwa na gazeti la Nyakati na kuizungumzia hiyo Helikopta akisema
‘kitendo cha Gwajima kununua helikopta kwa ajili ya kazi zake za Injili
kinastahili
kufurahiwa na Wakristo wote wa kweli, tujifunze kupongezana.. nampongeza sana’
‘Kumiliki
kwake Helikopta kutachangia katika kufuta dhana potofu ambayo imedumu
kwa muda mrefu ya kuyaita Makanisa ya kilokole…. makanisa ya
vichochoroni, Helikopta sio starehe na hata muundo wake sio wa starehe
bali ni kazi, itamwezesha pia kufika maeneo ambayo gari sio rahisi
kumfikisha kutoa neno la Mungu’ – Kakobe
Kuhusu
Askofu Kakobe kununua Helikopta yake, amesema >>> ‘mimi sio
mtu wa mashindano na pia kila mtu anakwenda sawa kutokana na ono
aliloitiwa, haya sio mambo ya kushindana… hicho ndicho kinacholeta shida
mara kwa mara, Gwajima ana Helikopta ni kwa manufaa ya Ufalme wa Mungu,
mimi nina chakwangu ni kwa utukufu wa Mungu, hakuna haja ya kuigana
No comments:
Post a Comment