Gari hilo lilikamatwa juzi saa 3:00 usiku katika Kijiji cha
Kigongoni katika Mji wa Mto wa Mbu, wilayani Manyara baada ya gari hilo
kupinduka.
Vyanzo vya uhakika kutoka ndani ya Jeshi na Polisi
zimeeleza kuwa askari wa jeshi hilo aliyekuwa akiendesha gari hilo
anashikiliwa na polisi.
Uchunguzi umebainisha kuwa ndani ya gari hilo kulikuwa na meno ya tembo na watu wengine watatu ambao walikimbilia porini na baadhi ya nyara hizo.
Uchunguzi umebainisha kuwa ndani ya gari hilo kulikuwa na meno ya tembo na watu wengine watatu ambao walikimbilia porini na baadhi ya nyara hizo.
Habari hizo zimedai bado kuna utata kuhusu gari
lililokuwa likitumiwa na maofisa hao kwa kuwa kibao cha namba za gari
hilo kinasomeka kwa namba za kiraia lakini vioo vimechorwa namba za
Serikali, huku Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa akisema pia kulikuwa na namba
za JWTZ.
Kulingana na taarifa kutoka ndani ya Jeshi la
Polisi, kukamatwa kwa gari hilo kulitokana na Askari wa Shirika la
Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Hifadhi ya Ziwa Manyara kudokezwa na
raia wema.
Inaelezwa kuwa baada ya askari hao kudokezwa,
walianza kufuatilia nyendo za maofisa hao ndani ya hifadhi na
walipogundua wanafuatiliwa, gari hilo liliongeza mwendo kuelekea Mji wa
Mto wa Mbu.
Hata hivyo, kutokana na mwendokasi wa gari hilo na kutokuwa wazoefu kulinganisha na Askari wa Tanapa, gari la maofisa hao lilipinduka lilipofika Kijiji cha Kigongoni nje kidogo ya Mto wa Mbu.
Hata hivyo, kutokana na mwendokasi wa gari hilo na kutokuwa wazoefu kulinganisha na Askari wa Tanapa, gari la maofisa hao lilipinduka lilipofika Kijiji cha Kigongoni nje kidogo ya Mto wa Mbu.
“Baada ya kupekuliwa lilikutwa na pembe mbili za
ndovu na uchunguzi wa awali umethibitisha maofisa waliokimbia
walifanikiwa kutoroka na pembe nyingine tatu,” kilidokeza chanzo hicho.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulitokana na wananchi kumtilia shaka yeye na wenzake gari lao lilipopata ajali kwa kitendo cha watu wawili waliokuwepo kwenye gari hilo kuonekana wakihamisha mizigo na kukimbilia porini.

“Matairi mawili ya gari yalipasuka lakini ajabu ni
kwamba wananchi walipojitokeza kusaidia majeruhi, wawili kati yao
walinyanyua mizigo isiyojulikana na kukimbilia porini huku wakimwacha
mwenzao aliyevaa sare za jeshi akisubiri garini,” alisema mtoa taarifa
wetu.
Kwa mujibu wa mashuhuda, wakati wa ajali hiyo,
mtuhumiwa alikuwa amevaa jaketi la JWTZ pamoja na suruali ya jinsi akiwa
na bunduki aina ya Rifle.
Katika msako uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na wananchi, pembe mbili zaidi za ndovu zilikutwa zikiwa zimefichwa karibu na eneo la ajali.
Katika msako uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na wananchi, pembe mbili zaidi za ndovu zilikutwa zikiwa zimefichwa karibu na eneo la ajali.
Mkurugenzi mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini akasema hana taarifa kamili
kwani yuko Tanga na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Mazingira.
“Ni kweli nimearifiwa juujuu tu, nasubiri taarifa
kamili lakini nimeambiwa tu hilo gari lilipinduka wakati wakifukuzana na
askari wetu, lakini mnaweza mkapata taarifa zaidi polisi,” alisema
Kijazi.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema hajapata taarifa hiyo, hivyo asingeweza kutolea maoni kwa namna yeyote.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment