Saturday, January 4, 2014

YANGA YAANZA KUJIFUA

mkwasa1 a63df
Mkwasa (mwenye jezi rangi za Bluu) akiongoza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa Bora Mabatini Kijitonyama
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu a Vodacom Tanzania Bara timu ya Young Africans leo imeeanza kujifua katika viwanja vya bora Mabatini Kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa.

Young Africans ilisimama kufanya mazoezi kwa siku takribani tatu kufuatia kufanya mabadiliko ya benchi la Ufundi na leo rasmi imeanza mazoezi asubuhi chini ya makocha wasaidzi Mkwasa na kocha wa makipa Juma Pondamali.
Mkwasa alitumia muda wa dakika 5 kuongea na wachezaji wote waliofika mazoezini siku ya leo, kuwaelekeza nini wanapaswa kufanya na kuzingatia mafunzo yake ambapo wachezaji waliweze kutekeleza kwa kiwango cha hali ya juu.
Kocha wa makipa Juma Pondamali aliwafua vilivyo magolikipa Juma Kaseja, Ally Mustafa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida" na kusema huu ni mwanzo tu kwani anaamini wachezaji hao watakua katika kiwango kizuri kutokana na uwezo wanaouonyesha katika mazoezi anayaowapatia.
Kikosi cha Young Africans kesho kitaendelea na mazoezi asubuhi katika uwanja wa Mabatini Kijitonyama ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili na mashindano ya kimataifa.

Aidha washambuliaji Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi waliokwenda kwao nchini Uganda kwa ajili ya matatizo ya kifamilia wanatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki tayari kuungana na wenzao kujiandaa na mzunguko wa pili.

No comments:

Zilizosomwa zaidi