MWANAMKE
ALIOFEFAHAMIKA KWA JINA LA ZAWADI AKIWA KITUO CHA POLISI STEND MJINI
MUSOMA
WANANCHI WAKITAFAKARI KUTOKANA NA TUKIO HILO
NJE YA KITUO CHA POLISI
MTOTO WA SIKU MOJA ALIYENUSULIKA KUIBWA
NI ULINZI MKALI KWA MTUHUMIWA
Mwanamke
mmoja aliyefahamika kwa jina la Zawadi Hamisi(22) mkazi wa Butimba
mkoani Mwanza amenusulika kuuwawa na Wananchi wenye hasira kali baada ya
kudaiwa kuiba mtoto mchanga wa siku moja kwenye hospitali ya mkoa wa
Mara.
Tukio
hilo limetokea majira ya saa 8 mchana maeneo ya barabara ya sokoni
Manispaa ya Musoma baada ya mwanamke huyo kumdanganya mzazi wa mtoto
huyo kuwa anaitwa na mama yake na kutumia mwanya huo kuondoka na mtoto
huyo kabla ya kusaidiwa na wasamalia wema kumkamata Mwanamke huyo.
Akizungumza
katika kituo kidogo cha polisi cha stendi ya zamani mjini
Musoma huku akibubujikwa na machozi, mzazi wa mtoto huyo Angelina Singu(22)
mkazi wa kijiji cha Masurura Wilayani Butiama alisema mwanamke
aliyedaiwa kumuiba mtoto huyo mwenye jinsia ya kiume alimwambia mama
yake yupo stend anamsubilia ili waondoke.
Alisema
alimfata akiwa hospitali ya mkoa wa Mara akijiandaa kuondoka baada ya
kujifungua septemba septemba 19 na kumueleza mama yake anamuita na
kumtaka msaidie mtoto ili waweze kumfuata na kuondoka kurudi nyumbani.
Angelina
alisema baada ya kutoka nje ya geti la hospitali ya walitembea hadi sted
ya zamani na baadae wakiwa umbali kidogo kutokana na mwendo wake kuwa
mdogo kutokana na uzazi alimuona mwanamke huyo akipanda pikipiki maarufu
kama bodaboda na kuanza kuondoka huku akimuacha.
Alisema
baada ya kuona hali hiyo aliamua kupiga kelele ya kuomba msaada ndipo
wasamalia wema pamoja na baadhi ya waendesha pikipiki walipoamua
kuifukuza pikipiki aliyopanda mwanamke huyo pamoja na mtoto aliyeibwa na
kufanikiwa kumkamata barabara ya sokoni.
"Inaonekana
huyu mwanamke alinifatilia pale hospitalini tangu nilipojifungua,hakuwa
na nia njema ni kweli alitaka kuondoka na mtoto wangu....masikini
nimeangaika miei tisa leo mtoto wangu anataka kuchukuliwa kwa kweli
nawashukuru walionisaidia ningekuwa kwenye hali gani mimi.
"Wanawake
tuoneane huruma hili sio jambo jema hivi karibuni nilisikia kwenye
vyombo vya habari mkoa mmoja kuna Mwanamke kaiba mtoto kumbe mambo haya
yapo imeniuma sana na namshukuru mungu na walionisaidia jambo hili na
vyombo vya sheria vichukue hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye
tabia kama hizi"alisema Angelina.
Mwanamke
anayedaiwa kufanya jaribio la kuiba mtoto huyo alisema alitoka Mwanza
kuja Musoma kwa ajili ya kumsalimia kaka yake na alikwenda hospitali ya
mkoa wa Mara kuchukua dawa kwa ajili ya matibabu.
Alisema
hakuwa na nia mbaya ya kuondoka na mtoto huyo bali alikuwa akimsaidia
kumbebea na alipooulizwa kwa nini aliamua kumuacha na kupanda pikipiki
peke yake alishindwa kuongea na alipoangaliwa kwenye mkoba wake alikutwa
na kadi ya ujauzito ikionyesha anatarajiwa kujifungua septemba 19 mwaka
licha ya kwamba alikuwa hana ujauzito.
Mmoja wa
mashusuda wa tukio hilo alisema alimuona mwanamke huyo aliyedaiwa kuiba
mtoto kwa siku mbili maeneo ya Nyakato Manispaa ya Musoma kama mgeni
karibu na nyumba anayoishi.
Kamanda
wa polisi mkoani Mara Ferdnand Mtui amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na Mwanamke anayedaiwa kufanya jaribio la kuiba mtoto anaendelea
kuhojiwa na jeshi la polisi na baada ya upelelezi hatua zaidi za
kisheria zitafuatwa.
No comments:
Post a Comment