Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kahama kwenye viwanja vya CDT na kuwaeleza mbinu chafu zinazofanyika kuvuruga mchakato wa Katiba. |
Katibu
wa NEC ya CCM itikadi na Uenezi amesema kinachowasumbua Chadema mpaka
wanafanya yote waliyoyafanya hasa ngumi na vurugu bungeni ni namna
watakavyoeleza kwa waliowapa pesa za kuvuruga mchakato wa katiba nchini
kwani wanatakiwa kupeleka mrejesho jinsi walivyofanikiwa na jinsi
walivyotumia mabilioni hayo.
Nape
ameyasema hayo kwenye mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kahama kwenye
ziara ya karibu siku ishirini kanda ya ziwa kwa mikoa mitatu yaani
Shinyanga,Simiyu na Mara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abralhaman
Kinana.
Kinana.
“Wenzetu
hawa nasikia wamepewa mabilioni toka nje kwa kisingizio cha kushiriki
mchakato wa katiba, na kama ilivyo kwa vibaraka wengine katika bara la
Afrika lengo la mapesa hayo sio kuwawezesha kushiriki bali kuanzisha
fujo na vurugu ili mchakato usimalizike salama iwe ajenda 2015 kwani
kimsingi hawana ajenda mpya” alisisitiza Nape.
Akielezea
swala la pesa kutoka nje Nape alisema mara tu baada ya rasimu ya kwanza
kutoka Katibu Mkuu wa Chadema alikwenda nje ya nchi na akakaa kwa muda
na aliporudi tu, ndio Chadema wakapanga kuanza kuzunguka na helkopta.
“Babu
atwambie alifuata nini nje? Na pesa za kuzunguka na misafara miwili
tofauti ya helkopta walitoa wapi? Na watwambie kama walisharudisha
mrejesho kwa wafadhili wao” alisema Nape
Nape
aliendelea kusisitiza kuwa yote yaliyotokea bungeni si mambo
yaliyotokea kwa bahati mbaya isipokuwa ni mambo yaliyopangwa na Chadema
katika mkakati wa kutimiza moja ya malengo yao.Alisema ilikua ni lazima
watafute mahali pa kufanya kituko bungeni ili iwe mjadala na ili wapate
sababu na picha za kuonyesha kwa waliowapa pesa kuwa wanapambana.
“hili
walilofanya Chadema bungeni ni jambo walilopanga katika mkakati wao wa
‘civil disobidiency’ …machafuko ya umma dhidi ya dola, mkakati ambao
unaratibiwa kutoka nje na baadhi ya wale waliokuwa wakoloni katika nchi
zetu za Afrika. Lengo ni kusababisha machafuko na nchi kutotawalika”
alisema Nape.
Nape
alisema ndio maana CCM ilisisitiza lazima bunge liendelee kuonyeshwa na
televisheni ili kuonyesha yanayoendelea bungeni kuwawezesha wananchi
kuona kinachofanywa na wawakilishi wao.
“bila
shaka wananchi mmeona kilichotokea bungeni kwa macho yenu, sina haja ya
kuwaeleza. Mmeona wabunge wa upinzani walichofanya,uchaguzi ujao
tupunguze idadi ya vichaa bungeni ili kodi zetu zitumike vizuri,kwani
tuliwatuma wakajadili maendeleo yetu wao wamegeuza bunge uwanja wa
masumbwi.
Aidha
Nape akifafanua hoja ya upinzani bungeni juu ya idadi ya wabunge wa
bunge maalum la katiba alisema upinzani hawana hoja ya msingi bali
wanasukumwa na ubinafsi na ulafi wa madaraka.
“Hoja iliyowafanya wapigane bungeni haina mashiko, wanataka idadi iongezwe ya wabunge wa bunge la katiba kutoka 357 mpaka 792.
Hivi nani anabeba mzigo huu wa kuwalipa hawa wabunge kama sio mwananchi wa kawaida? Halafu mnajiita watetezi wa wanyonge? Hamuoni aibu?” alihoji Nape.
Hivi nani anabeba mzigo huu wa kuwalipa hawa wabunge kama sio mwananchi wa kawaida? Halafu mnajiita watetezi wa wanyonge? Hamuoni aibu?” alihoji Nape.
Akiendelea
kufafanua Nape anasema, ” katika hali ya kawaida tungetegemea wajenge
hoja ya kundi kubwa katika jamii ya kitanzania ambao ni wakulima na
wafanyakazi ndio wawe na uwakilishi mkubwa kwenye hilo bunge kama
tunataka katiba kweli ya wananchi lakini badala yake wao wanapendekeza
wawakilishi kutoka vyama vya siasa ukiacha wabunge waliopo sasa wawe 72
na wakulima wawe 10 tu! Wanataka katiba ya vyama vya siasa badala ya
katiba ya nchi kwa ajili ya wananchi.
Wanataka wafugaji wawe 10 tu na wafanyakazi 40. Kwa uwiano wa kawaida asilimia 80% wa wananchi wa nchi hii ni wakulima, tungetegemea wangependekeza idadi yao kuwa kubwa lakini wao wanawapuuza wakulima na wafugaji kwa kudai wawe kumi tu”!
Wanataka wafugaji wawe 10 tu na wafanyakazi 40. Kwa uwiano wa kawaida asilimia 80% wa wananchi wa nchi hii ni wakulima, tungetegemea wangependekeza idadi yao kuwa kubwa lakini wao wanawapuuza wakulima na wafugaji kwa kudai wawe kumi tu”!
Nape alimalizia kwa kudai kuwa siku za vyama kama Chadema zinahesabika maana hii ya katiba ndio ilikuwa karata yao ya mwisho.
”
Nimalizie kwa kuwatahadharisha vijivyama hivi vingine kama CUF, NCCR
mageuzi na wengine kuwa wenzao wamepewa mapesa wao wanwaunga mkono kwa
ajenda iliyojificha. Na kwakuwa hili la kuvuruga katiba ndio karata yao
ya mwisho basi tutarajie anguko baya sana kwa Chadema na huo ndio
utakuwa mwisho wao”!alimalizia Nape.
No comments:
Post a Comment