Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela akitoa taarifa
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kijana mmoja mkazi wa
Kibaoini Singida mjini, kulawitiwa na rafiki yake baada ya kulewa pombe
ya viroba aina ya jogoo.(Picha na Nathaniel Limu).
‘Ulevi
noma’ hiyo imedhihirika baada vijana wawili wa kiume marafiki kunywa
pombe nyingi na kuepelekea mmoja amwingilie kimwili kinyume na maumbile
rafiki yake kipenzi.
Inadaiwa
Athumani Juma mkazi wa Kibaoni alimwingilia kimwili kinyume na maumbile
rafiki yake wa kiume mwenye umri wa miaka 26 (jina tunalo).
Kamanda
wa polisi wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema tukio hilo la aina
yake, limetokea Agosti 27 mwaka huu saa tatu usiku eneo la soko la
Kibaoni kata ya Kindai mjini Singida.
Amesema
siku ya tukio, marafiki hao walikutana dukani ambapo mtuhumiwa Athumani
alinunua viroba vinne aina ya jogoo, huku muathirika akinunua viroba
tisa.
Kamanda
Kamwela amesema baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake,
muathirika alitangaza kuwa amelewa na hivyo kila mmoja arejee nyumbani
kwao.
Kamanda
kamwela amesema “Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika
alimwambia rafiki yake Athumani kuwa amwache hapo ili aweze kupumzika
kwa vile pombe ilikuwa imemzidi sana, lakini ghafla alianguka chini na
kisha kuzirai na kupoteza fahamu”.
Amesema
kuwa baada muathirika kupoteza fahamu, mtuhumiwa Athumani alitumia
fursa hiyo na kuanza kumwingilia kimwili rafiki yake kinyume na
maumbile.
Amesema
wapita njia waliweza kushuhudia Athumani akiendelea na unyama wake huo
dhidi ya rafiki yake, lakini walipojaribu kumkamata, aliweza
kuwaponyoka na kukimbilia kusikojulikana.
Kamnda
huyo ameongeza kuwa “Raia wema walimbeba muathirika na kumpeleka hadi
nyumbani kwao na baadae aliweza kupata fahamu na ndipo aliposikia
maumivu makali kwenye sehemu yake ya haja kubwa”.
“Baada
ya muathirika kusikia maumivu makali, alikimbizwa hospitali ya mkoa na
baada ya uchunguzi, alibainika ameharibiwa vibaya sehemu yake ya siri
ya kutolea haja kubwa”.
Kamwela
amesema kwa sasa wameanzisha msako mkali wa kumsaka Athumani, ili
waweze kumkamata na kumfikisha mbele ya mahakama kujibu tuhuma
inayomkabili.
No comments:
Post a Comment