Friday, August 16, 2013

BARCELONA KUTETEA TAJI LAO WAKIWA NA HOFU ....

Barcelona watajitupa dimbani Jumapili kuanza harakati za kulitetea taji lao la ligi kuu nchini Hispania huku wakiwa na hofu juu ya ubora wa mchezaji Neymar kuweza kulizoeaa na kulimudu soka la barani Ulaya. 
Kitu kingine ni jinsi kocha mpya Gerardo 'Tata' Martino atakavyoweza kuonesha uwezo wake na kuipa mafanikio Barcelona kama ilivyokua kwa makocha waliopita.

Kocha huyu Muargentina aliteuliwa mapema mwezi uliopita kuchukua nafasi ya Tito Vilanova  msaidizi wa zamani wa Pep  Guardiola kutokana na matatizo ya kiafya yaliyomfanya kuachia ngazi na  kushindwa kuendelea kuinoa timu hiyo Ingawa uteuzi wake haukutegemewa na wengi.
Kocha huyu kabla ya kujiunga na Barcelona alikua akiinoa timu ya zamani ya Lionel Messi ya Newell's Old Boys.

Barcelona imewapoteza nyota wake akiwemo straika David Villa aliyejiunga na Atletico Madrid, pamoja na Thiago Alcantara aliyetimkia Bayern Munich. Mabingwa hao wa Hispania wametumia €57 million kumnasa kinda wa Kibrazil Neymar mwenye umri wa miaka 21.
Neymar mefunga magoli mengi wakati wa mechi za majaribio na ameonekana akizoeana vizuri na wachezaji wenzake. Kinda huyo ameahidi kufanya vizuri na kuonesha ubora wake zaidi.
Na Mligo G

No comments:

Zilizosomwa zaidi