Friday, August 16, 2013

KIVUMBI YANGA, AZAM KWENYE NGAO YA JAMII.....

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga Sports Club na makamu bingwa Azam FC wanatarajia kuvaana kesho (Jumamosi) kwenye mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa 2013/2014. 

Mechi hiyo  itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni ambapo mshindi atakabidhiwa ngao. 

Iwapo dakika 90 za mechi hiyo hazitatoa mshindi, timu hizo zitatenganishwa kwa mikwaju ya penalti huku asilimia 10 ya mapato ya mechi hiyo yakienda kwa kituo cha kulelea watoto cha SOS. 

Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu wakati viti vya rangi ya chungwa ni Sh10,000. Watakaiongia viti Maalum yaani  VIP ( C) watalipa Sh15,000, viti vya VIP (B) ni Sh20,000 wakati VIP (A) watalipa Sh30,000. 
Na Mligo G

No comments:

Zilizosomwa zaidi