Thursday, August 15, 2013

DROGBA AREJEA TIMU YA TAIFA KWA MBWEMBWE....

DidierDrogba atua na goli katika timu ya taifa baada ya jana kuifungia timu yake bao pekee la kufutia machozi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Mexico huko New York. Drogba akitokea benchi kipindi cha pili alipiga faulo ambayo ilizuiwa na Gerrardo Torrado na mwamuzi kuamulu penalty, bila ajizi Drogba  alifunga mkwaju huo wa penalti kwenye mchezo ulioisha kwa Mexico kuibuka kwa ushindi mnono wa mabao 4-1.

Ingawa matokeo hayo yameonekana kama aibu kwa timu inayoshika nafasi ya kwanza kwa ubora barani Africa, tembo hao waliwakosa baadhi ya wachezaji wao nyota akiwemo Yaya Toure ambaye ndiye mchezaji bora wa mwaka barani Africa. Kocha Ivory Coast Mfaransa  Sabri Lamouchi aliwaacha benchi baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa, hadi pale walipoingizwa madhara yalikuwa yamekwisha igharimu timu. 

Baada ya kuondoka Chelsea na kwenda China kulimgharimu Drogba kutokana na kiwango kidogo cha soka eneo hilo, hali iliyopelekea kuonesha kiwango cha chini wakati wa michuano ya kombe la mataifa Africa mwanzoni mwa mwaka huu nchini Afrika Kusini. Mara baada ya kushindwa kuchukua kombe hilo kitu cha kwanza alichokifanya kocha Lamouchi ilikua ni kumwacha Drogba katika kikosi chake na kumwambia aboreshe kiwango chake. 

Drogba ameonekana kurudi katika kiwango chake hasa baada ya kutoka nchini China na kutimkia Uturuki kitu kilichomfanya kocha Lamouchi kumjumuisha kwenye kikosi cha jana katika mechi ya kirafiki. Bila shaka sasa Drogba anamatumaini ya kuiitwa tena kikosini kuelekea mpambano wao dhidi ya Morocco mwezi Septemba kuwania kufuza kucheza fainali za kombe la Dunia nchini Brazil hapo mwakani.
Na Mligo G.


No comments:

Zilizosomwa zaidi