Baada ya kutumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vitano
vya Bunge, wabunge watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), jana waliingia bungeni wakionekana kuwa na ari mpya.
Wabunge waliosimamishwa Aprili 17 ni Mnadhimu Mkuu
wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Wengine ni Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiel Wenje
(Nyamagana), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini) na Godbless Lema
(Arusha Mjini).
Jana asubuhi Mchungaji Msigwa alikuwa miongoni mwa
wabunge waliowahi kuingia mapema ndani ya Ukumbi wa Bunge na kufuatiwa
na Lissu muda mfupi baada ya kikao kuanza.
Ndani ya Ukumbi wa Bunge, Msigwa alipata nafasi ya
kuuliza swali namba 115 lililokuwa liulizwe na Joyce Mukya kuhusu
Kampuni ya Kamwene Woodworks . Kwa upande wake, Lissu aliomba mwongozo
wa Spika kuhusu kukwama kwa Bajeti ya Wizara ya Maji.
Wabunge wengine haikujulikana sababu za kutofika jana licha ya kuwa adhabu yao ilikwisha tangu April 25 huku taarifa zikieleza kuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema alikuwa apelekwe mahakamani kujibu staka la uchochezi.

No comments:
Post a Comment