Ofisi ya Rais wa Rwanda imekanusha vikali uvumi ulioenea
nchini humo na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwamba
Rais Paul Kagame wa nchi hiyo amefariki dunia.
Taarifa zinasema kuwa,
uvumi wa habari za kufariki dunia Rais Kagame, zimeamsha furaha hasa kwa
wakaazi wa miji ya mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo.
Mara kadhaa Rwanda imekuwa ikituhumiwa kwa uingiliaji wa kijeshi
katika maeneo ya mpaka na Kongo. Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulitoa
taarifa na kuituhumu tena serikali ya Kigali kwa kuyaunga mkono makundi
yanayobeba silaha na hasa waasi wa zamani wa M23 waliokuwa mashariki mwa
Kongo.
Hata hivyo ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imekosolewa vikali na
serikali ya Rwanda. Rais Paul Kagame mwenye umri wa miaka 56 aliiingia
madarakani mwaka 1994, baada ya kutokea mauaji ya kimbari yaliyopelekea
watu wasiopungua laki nane hasa wa kabila la Kitutsi kuuawa nchini humo.
No comments:
Post a Comment