Shirika
la nyumba la Taifa NHC limekiri kwamba ndio mmiliki wa kiwanja
kilichokua kimejengwa jengo la gorofa 16 ambalo liliporomoka siku kadhaa
zilizopita Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu 36 na kujeruhi
18.
Mkurugenzi
Mkuu Nehemia Mchechu amesema kwa kawaida shirika la nyumba limekua
likiingia ubia na watu binafsi wenye uwezo wa kujenga nyumba kama hizo
ambapo liliingia ubia na kampuni ya ujenzi ya RAZA na kusaini mkataba wa
kujenga jengo lenye gorofa 10 tu kwenye eneo hilo ingawa baadae kampuni
hiyo iliomba kubadili mkataba ili wajenge gorofa 16.
Kuhusu
umiliki kwa asilimia 25 kwenye jengo lililoporomoka, Mchechu amesema
kwa ubia uliokuwepo walipaswa kupewa asilimia hizo baada ya ujenzi
kukamilika na asilimia nyingine 25 wangepewa miaka kumi baadae kulingana
na mkataba na hawakupaswa kuhusika kwenye gharama zozote wala taratibu
za ujenzi.
Asema “february 15 2011 ndio walituandikia kwamba wanakusudia
kuongeza gorofa zifike 16 na kwamba wanawasiliana na Mamlaka husika kwa
ajili ya kupata vibali hivyo na wakifanikiwa wangeomba kuongezewa muda
wa kumaliza mradi na pia baada ya kupata kibali wangetutaarifu kwa ajili
ya kufanya marekebisho ya mkataba”
Kwenye
line nyingine, NHC imeunda timu kwa ajili ya kufanya ukaguzi katika
miradi yake yote ya ujenzi wa ubia ili kujihakikishia usalama wa majengo
husika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
-
-
Kaimu Mkurugenzi wa SUMATRA Athman Kilima akizungumza na waandishi wa habari leo April 02,2013 katika makao m...
-
Manfred Adam anayekabiliwa na kesi ya kutishia kuua katika hali isiyotarajiwa amelimwaga kojo katika Mahakama ya Mwanzo na kuleta vurugu ...
-
MTUHUMIWA wa mauaji ya watu tisa na unyang'anyi wilayani Tarime mkoani Ma...
No comments:
Post a Comment