Hii ndio kauli iliyotolewa
na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe
kuhusu kilichoandikwa na gazeti la Mtanzania march 13 2013 toleo namba 7255.
“SAKATA LA KUTESWA KWA KIBANDA:
Membe atajwa” na kwamba eti mimi ninahusika na vitendo vya kikatili na
unyama alivyofanyiwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa kampuni ya New Habari, Bw.
Absalom Kibanda”
“Nimeshangazwa na kusikitishwa
sana na habari hizo na ningependa kuwahakikishia Watanzania wenzangu
kwamba sijahusika, sihusiki na sina sababu ya kuhusika kwa namna yoyote
ile. Sina nia, genge wala fedha za kufanya shughuli kama hiyo. Katika
maisha yangu yote, sijawahi kugombana naye na hajawahi kunifanyia ubaya
wowote. Kwa kifupi, sina uhasama na Bw. Absalom KIbanda”
“Nawashukuru sana wananchi wenzangu, jamaa na marafiki walioniletea salamu za kunitia moyo. Naungana nao katika kujiuliza, hivi kiburi hiki, dhihaha hii na ujsriri huu wa kusema uongo hadharani wanautoa wapi!? Jeuri na kiburi cha nmana hii hakiwezi kutokana na sheria za nchi, haki ya kikatiba wala hofu ya Mwenyezi Mungu. Naomba Watanzania wenzangu mnisaidie kutegua kitendawili hiki. Naamini kwa dhati kwamba ukweli kuhusu suala hili utajulikana na yeyote mwenye ushahidi wa kweli aonyeshe uzalendo wake kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama”
“Mwisho, wakati nashauriana na wanasheria wangu kuona hatua ya kuchukua dhidi ya kuchafuliwa huku, nawaomba Watanzania wenzangu tuvute subira na tuache vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi zake ili Watanzania hatimaye wajue ukweli wa kilichotokea”
No comments:
Post a Comment