SAKATA
la mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha
Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi limezidi kuchukua
sura mpya baada ya askari waliomfikisha mtuhumiwa huyo wa mauaji
askari wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23)
kumtibua hakimu na kuageza mtuhumiwa huyo kurudishwa tena kizimbani kwa
kudharau mahakama hiyo.
Tukio
hilo lilitokea leo majira ya saa5.35 kwa askari hao watatu ambao
majina yao hayakuweza kufahamika mara moja kumshusha kizimbani
mtuhumiwa huyo wa mauwaji na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa
kupigwa picha na wanahabari waliokuwepo hapo lilitokea mara baada ya
mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo.
Huku
bado mahakama ikiwa inaendelea kwa hakimu kutaja tarehe ya kesi hiyo
namba ya mauwaji kesi namba 1 ya mwaka 2012 mtuhumiwa wa mauwaji
alishuka kizimbani huku akivaa kofia yake ya sweta (mzula)na miwani ya
giza na kuanza kushuka jukwaani kabla ya hakimu kumtaka mtuhumiwa huyo
kutovalia kofia hiyo kizimbani huku kabla ya mahakama kumalizika.
Wakati
hakimu huyo akijiandaa kusimama ili kuhitimisha shughuli za kimahakama
kwa siku hiyo ghafla alijikuta anabaki na mwanasheria wa mahakama
,kalani wake ,wanahabari ,askari mmoja na ndugu wawili wa mtuhumiwa
huyo huku askari watatu wenye silaha na mtuhumiwa huyo wakiwa tayari
wameondoka ndani ya chumba cha mahakama hiyo.
“Mbona
hao askari wanamtoa mtuhumiwa bila utaratibu wa mahakama hebu
mwanasheria waambie wamrudishe ndani mtuhumiwa ....huu si utaratibu
mbona wanafanya fujo mahakamani hao” alisikika akisemahakimu mkazi
wilaya ya Iringa Dyness Lyimo
Hata
hivyo pamoja na jitihada za mwanasheria wa serikali Adolf Maganda
kuwaita kwa sauti askari hao kuwataka kumrudisha ndani ya mahakama
mtuhumiwa huyo bado askari hao walizidi kukimbia na mtuhumiwa kwenda
nae mahabusu na baada ya dakika kama 5 hivi ndipo mwanasheria huyo
aliporejea na askari hao na mtuhumiwa ambae hata hivyo hakwenda
kusimama kizimbani na badala yake alikwenda upande wa kushoto wa
mahakama hiyo ambako alikuwa amekaa mwanzoni kabla ya mahakama kuanza
na kuketi katika kiti huku akiwa amevaa miwani na kofia yake.
Kutoka
na tukio hilo hakimu huyo alilazimika kuwahoji askari hao watatu
kwa vurugu hizo walizozifanya kwa kuwauliza swali moja pekee kuwa
wanaona walichofanya ni sahihi na askari hao kuomba msahama kuwa
samahani mheshimiwa.
Mwendesha
mashtaka wa jamhuri Adolf Maganda aliiomba mahakama hiyo kutaja tarehe
nyingine ya kutajwa tena kesi hiyo ambayo ilitajwa Januari 27 na
mtuhumiwa huyo kushindwa kufika kutokana na tatizo la ugonjwa
lililokuwa likimsumbua .
Hata
hivyo mahakamani hiyo liahirisha kesi hiyo hadi Februari 14 mwaka
huu kesi hiyo itakapofikishwa mahakani hapo kwa kutajwa tena.
Mtuhumiwa
huyo anatuhumiwa kumuua kwa bomu aliyekuwa mwandishi wa habari wa
Chanel Tena mkoa wa Iringa marehemu Mwangosi septemba 2 Septemba
mwaka jana katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa
wakati wa vurugu kati ya polisi na wafuasi wa Chadema .kinyume na
kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.
Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16
iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002,
Na Francis Godwin
Na Francis Godwin
No comments:
Post a Comment