Kama
ni kituko cha mwaka basi hiki pia ni kituko cha aina yake pamoja na
diwani wa kata ya Ifunda jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa mkoani
Iringa Mheshimiwa Elia Mgwila kufumaniwa na kukatwa sikio moja na
kung'olewa meno ila bado diwani huyo ambae ni majeruhi ameendelea
kugoma katukatu kwenda Hospital kutibiwa majeraha hayo.
Mbali
ya kuwagomea ndugu na marafiki hao bado diwani huyo amegoma kwenda
kituo cha polisi kufungua shitaka hilo na kudai kuwa yote anamwachia
mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyopo duniani .
Wakati
diwani huyo akigoma kufika Hospital kutibiwa taarifa zinadai kuwa
jeshi la polisi ambalo lilikuwa likimshikilia bwana mwenye mke
aliyefumaniwa na diwani huyo mkazi wa kijiji cha Ifunda kibaoni pamoja
na mdogo wake na mkewe wameachiwa huru na jeshi la polisi ambalo
lilikuwa likiwashikilia kwa tukio hilo la kumjeruhi diwani .
Huku
habari za kipolisi zikidai kuwa watuhumiwa hao wameachiwa huru
kutokana na diwani huyo kugoma kufungua kesi juu ya shambulio hilo
la mwili.
Diwani Elia Mgwila aliyesimama |
Mpiga kura akigonga mlango wa diwani bila mafanikio |
Nyumba ya aliyofumaniwa diwani huyo na mke wa mtu hii hapa
Hapa ni nyumbani kwa mheshimiwa mlango ukiwa umefungwa huku ufunguo ukiwa nje |
Mwananchi akitoka kumwona diwani huyo bila mafanikio leo
No comments:
Post a Comment