Wednesday, December 12, 2012

MKURUGENZI MTENDAJI BUNDA AZOMEWA.

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bunda, Dinah Rweyemamu juzi alipatwa na wakati mgumu pale alipozomewa na wananchi wakimshinikiza ashuke jukwaani kufuatia wananchi hao kutoridhika na majibu aliyokuwa akiyatoa kwa maswali yao.
Dinah alifikwa na zahama hiyo muda mfupi baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Abdallah Bulembo kumwita jukwaani ajibu maswali hayo yaliyoelekezwa kwake  wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyikia katika eneo la kituo cha zamani cha mabasi mjini Bunda.
Swali lililomletea kizaazaa kaimu mkurugenzi huyo ni lile lililotolewa na Alfred Ndowa aliyetaka kujua sababu za kukithiri kwa michango kwa shule za msingi na sekondari hasa wakati wa kuandikisha wanafuzni wa darasa la kwanza.
Bulembo alimwita Dinah jukwaani ambapo katika kujibu alisema dhamana ya kutokuwapo au kuwapo kwa michango mashuleni imo mikononi mwa kamati zao za shule.Kufuatia kauli hiyo ,wananchi walianza kumzomea kaimu mkurugenzi huyo wakisema hajui kitu na kumtaka Bulembo amshushe.

No comments:

Zilizosomwa zaidi