Rwanda iliwasilisha ombi la kutaka Kanali huyo
Laurent Serubuga, wa kabila la Hutu, na ambaye alihudumu kama naibu mkuu
wa majeshi kurejeshwa nchini humo.
Kanali Serubuga mwenye umri wa miaka
77, alikamatwa mwezi Julai Kaskazini mwa Ufaransa baada ya Rwanda kutoa
kibali cha kumkamata.
Takriban watu 800,000 wengi wao wakiwa wa kabila
la Tutsi, waliuawa na wahutu ambao ni wengi kwa idadi nchini Rwanda
mnamo mwaka 1994.
Mwanawe Serubuga alikuwa mahakamani kushuhudia
kesi hiyo. Wakati jaji akitoa uamuzi wake, alisema kuwa wameridhishwa na
uamuzi wa kumwachilia huru babake.
"tulirajaria kesi ya kisiasa. Uongo wa Rwanda
haujasikika mbele ya mahakama hii," alinukuliwa akisema na shirika la
habari la AFP .
Mahakama iligundua kuwa wakati wa mauaji ya
kimbari, uhalifu wa mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu
haungeweza kuadhibiwa chini ya sheria ya Rwanda, kwa hivyo, bwana
Serubuga hangeweza kuchukuliwa hatua zozote kwa makosa ambayo hayakuwa
na adhabu.
Sheria za Ufaransa, haziruhusu mshukiwa au
mhalifu kurejeshwa kwao hasa ambapo mshukiwa ana wasiwasi ikiwa haki
zake zinaweza kulindwa, alisema wakili wa Bwana Serubuga.
Wakili aliyekuwa anatetea maslahi ya Rwanda
alisema kuwa hakushangazwa na uamuzi huo kwani Ufaransa mara kwa mara
imekataa kuwarejesha washukiwa wa mauaji hayo nchini Rwanda ili
wakabiliwe na sheria.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment