Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kulima shamba la mpunga kwenye mradi wa kilimo kwanza wa Skimu ya Mahenge.
Mifereji ya maji kwenye shamba la skimu ya Mahenge
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyeka majani kwenye eneo la soko la sabasaba mjini Korogwe.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kujenga zahanati Mahenge kwa Mndolwa.
Mbunge wa Korogwe mjini Bw.
Yusuph Nassir akielezea mipango ya maendeleo ya jimbo lake wakati wa
kukagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya Mahenge Kwamndolwa .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa vyumba vya maabara vya shule ya sekondari ya Old Korogwe.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Korogwe kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi
ambapo aliwaasa vijana kuwa makini na wanasiasa wanaotanguliza madaraka
kuliko utu.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa Korogwe
kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi hao kuchagua
viongozi bora kwenye chaguzi zote zijazo,kuhakikisha watoto wao wanaenda
shule na wasirudishwe kwa sababu ya ada na mwisho aliwasisitiza wakazi
wa Korogwe kujiunga na mifuko ya Afya ya jamii.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Korogwe
Mheshimiwa Mrisho Gambo kusalimia wananchi wa Korogwe wakati wa mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Mazoezi.
Mkuu wa Wilaya
ya Korogwe Mheshimiwa Mrisho Gambo akiwahutubia wakazi wa Korogwe wakati
wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi ya
Mazoezi.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Korogwe kwenye mkutano
uliokuwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa na shauku ya kuuliza maswali
kuhusu maendeleo yao ya Korogwe.
No comments:
Post a Comment