Watu
10 wamekufa papo hapo mmoja kufariki
akiwa hospitali na wengine 30 kujeruhiwa
vibaya kufuatia ajali mbaya ya Basi la
Luhuye Express lililokuwa likitoka wilayani Tarime mkoani Mara kuelekea Jijini
Mwanza.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa njia
ya simu na Kamanda wa
Polisi
mkoa wa Simiyu,Kamishina Mwandamizi wa Polisi(SACP)Charles
Mkumbo
zinaeleza kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 5:11 asubuhi
katika
kijiji cha Itwimila wilayani Busega.
Alisema
kuwa basi hilo lenye namba za usajili T 410 AWT liliacha njia
na kugonga nyumba ya Marehemu ,Mwalimu Lazaro Mbofu na kuibomoa
yote
na kisha kupinduka .
Kamanda
Mkumbo alisema hadi sasa wametoa miili ya watu 10 katika basi
hilo
na majeruhi zaidi 30 wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya
Bugando
kwa matibabu zaidi.
“Hadi
sasa kuna maiti 10 zilizopatikana eneo la tukio na zaidi ya watu
30
wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Bugando kwa ajili ya
matibabu
ila taarifa kamili nitaitoa baadaye juu ya watu waliokufa na
waliojeruhiwa
kwani sasa nimetuma askari wa usalama barabarani
kufuatilia”alisema.
Mmoja
wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo,Juma Ally mkazi wa kijiji
cha
Itwimila akiongea na Mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema kuwa
aliona
basi hilo likiwa kasi na kupoteza mwelekeo na kutoka barabarani
na
kisha kuigonga nyumba hiyo na kuipita
juu ya paa na kupinduka.
“Niliona
Basi hilo lililokuwa likitokea barabara ya Musoma kuelekea
Mwanza
likiwa katika mwendo wa kasi na dereva nadhani alishindwa
kulimudu
na kasha kutoka nje ya barabara ya kuigonga nyumba na kisha
likapita
juu ya nyumba hiyo na kisha kupinduka”alisema.
No comments:
Post a Comment