
Mahakama ya juu zaidi
nchini India imetoa uamuzi wa kihistoria unaotambua watu waliobadilisha
jinsia yao kama watu wa kawaida katika jamii.
Kawaida kuna jinsia mbili, mke au mume
lakini mahakama hiyo imesema kuwa watu wanaoamua kubadilisha jinsia yao
kuambatana na hisia zao pia ni lazima watambuliwe na jamii na walio
katika aina ya jinsia kivyao.
Mfano wa watu kama hao ni mtu
anayezaliwa kama mwanamke lakini anahisi kisaokolojia kuwa yeye ni
mwanaume na hivyo hubadilisha jinsia yake na kuwa mwanamume kwa hata
kufanyiwa upasuaji.
Uamuzi huu wa mahakama bila shaka ni
wa kihistoria na unasema watu hao wasio jitambua kama wanaume au
wanawake wanaruhisiwe na kutambulika kama wanavyotaka
Katika kitambulisho chao
hawatajulikana kama wanaume au wanawake bali 'Transgender' kama jinsia
ya tatu, sio wanaume wala wanawake.
"ni haki ya kila binadamu, kuchagua jinsia wanayoitaka,'' alisema jaji katika uamuzi huo ambao unawapa watu hao haki ya kujitambulisha kama wanaume au wanawake
Iliamuru serikali kuwapa watu hao
nafasi za kazi na elimu kama jamii ya watu waliotengwa. Mahakama pia
imeitaka serikali kuwapa huduma muhimu watu hao wanaochagua
kujitambulisha watakavyo.
Takwimu zinasema kuwa watu milioni mbili nchini India wamebadilisha jinsia yao.
Wanaharakati wanasema kwamba, watu hao
wanatengwa na kuishi katika umaskini mkubwa na pia wanachukiwa kwa
sababu ya kubadilisha jinsia yao.
Wengi hujikimu kimaisha kwa kuwa waimbaji , kuombaomba barabarani na kujihusisha na biashara ya ngono.
Kadhalika wanaharakati wanasema kuwa watu hao hunyimwa huduma za matibabu hospitalini.
''Watu hawa ni raia wa India na lazima waheshimiwe na kupewa nafasi ya kunawiri maishani,'' alisema jaji katika uamuzi wake.
"lengo la katiba ni kuhakikisha kila
mtu wa India anapewa nafasi ya kuishi vyema na kujiendeleza maishani,
licha ya jinsia , dini na jamii anakotoka(Awadh Ibrahim)
No comments:
Post a Comment