
Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefuye ametoa taarifa hizi
huku akionyesha hati hiyo ya muungano Ikulu hapo jana April 14 2014 Dar es
salaam akianza kwa kusema ‘siku
12 zijazo tutakua tukisherehekea sikukuu ya muungano wa Zanzibar na
Tanganyika na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’
‘Inasikitisha sana kuwa leo miaka 50 baadae ipo dhana potofu
inayojengwa kuwa Muungano huu si halali kwa vile hakuna hati ya
Muungano,waasisi wa taifa letu ambalo tarehe 22 April 1964 kule Zanzibar
walitia saini hati hiyo mbele ya mashuhuda nao wameonekana kama
walichokifanya kilikua ni kiini macho’
‘Kwa hiyo waliongoza taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa msingi wa kiini macho hiko kwa miaka yote hadi mwenyezi Mungu
alipowachukua,mambo yote mawili yametusononesha sana wananchi
wanaoipenda nchi yao wanaoipenda waasisi wa nchi yao na wanaouenzi
Muungano wetu’
‘Ukweli ni kuwa hati hiyo ipo na ilikuwepo siku zote hata hivyo
lazima tukubaliane kuwa zipo hati fulani ambazo ni kiini cha uwepo wetu
kama taifa huru,kama jamhuri huru,kama muungano huru ambazo
tunazihifadhi kama mboni ya jicho’
‘Hati hizo ni pamoja na hati ya Uhuru wa Tanganyika ya mwaka
1961,hati ya Tanganyika kuwa Jamhuri mwaka 1962 na hatimaye hati ya
Muungano ya Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964,hati za namna hii
zinahifadhiwa maeneo maalum ambayo ni salama ili zisipotee wala
kuharibika,kwa kawaida hatuzitoi tunazifungia ili kuzihifadhi’.
No comments:
Post a Comment