Serikali ya Nigeria inasema kuwa
iko tayari kuzingatia mbinu zote zitakazowezesha kuachiliwa huru salama
kwa zaidi ya wasichana mia mbili wa shule waliotekwa nyara na
wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Awali waziri wa serikali alikuwa ameshikilia
msimamo mkali kama vile kukatalia mbali pendekezo la kiongozi wa Boko
Haram la kubadililishana wafungwa wa Boko Haram wanaozuiliwa na serikali
na wasichana hao.
Wakati huohuo, jamaa namarafiki wa wasichana hao waliotekw anyara
wameweza kuwatambua baadhi ya wasichana kutoka katika kanda ya video
iliyotolewa na kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekahu siku ya Jumatatu.
Familia za wasichana hao ziliweza kutazama kanda
hiyo ambapo Shekahu alisema sharti serikali iwaachilie wafungwa wao
kabla ya wao kuwaachilia wasichana hao ambao kundi hilo limesema
wameweza kuwasilimisha.
"Ni heri watuonyeshe maiti za wasichana wetu badala ya kuwazuilia vichakani. Hili ni swala la hisia za binadam. Sisi hatuwezi kwenda kuwaokoa, wanajeshi hawawezi kwenda huko. Ni heri kutumia nguvu. Tukiona maiti zao mioyo yetu itakua huru"
Marekani imesema inapeleka vifaa vya uchunguzi
nchini Nigeria kusaidia katika juhudi za kuwatafuta wasichana
wanaozuiliwa na kundi la Boko Haram.
Wasichana hao walitekwa nyara kutoka shule moja Kusini mwa eneo la Borno mwezi mmoja uliopita.
Msemaji wa Rais Obama Jay Carney amesema kikosi cha maafisa 30 kiko nchini Nigeria tayari kushiriki juhudi hizo.
Amesema msaada huo wa Marekani kutoka wizara za mambo ya nje na ulinzi na pia kutoka idara ya uchunguzi ya FBI.
Hatua hiyo imechukuliwa wakati baadhi ya Jamaa
za wasichana waliotekwa nyara wakielezea majonzi baada ya kutazama kanda
ya video iliyotolewa na kundi hilo.
Baadhi wameiambia BBC kuwa kanda hiyo imewapa
matumaini lakini wameshangaa kuona wasichana hao ambao wengi ni Wakristu
wamevalia mavazi ya Kiislam.
Akizungumza kwa uchungu nduguye mmoja wa
wasichana waliotekwa ameiambia BBC ni heri kanda hiyo ingeonyesha maiti
za wasichana hao kwa kuwa hiyo ingeondoa wasiwasi unaoendelea kukithiri
na kuumiza mioyo ya wengi.
Kwenye kanda hiyo ya video kiongozi wa Boko
Haram , Abubakar Shekau anasikika akiambia serikali ya Nigeria yuko
tayari kubadilishana baadhi ya wasichana hao na wafuasi wake waliofungwa
jela.
Seneta Ali Ndume kutoka eneo ambapo wasichana hao walitekwa nyara anaisihi serikali kulegeza msimamo.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment