Friday, April 11, 2014

MAANDALIZI KUMBUKUMBU YA SOKOINE YAKAMILIKA'

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kushoto) akimsikiliza Waziri Mkuu wake (enzi hizo) Edward Moringe Sokoine kabla ya kuanza kwa mojawapo ya vikao vya kiserikali.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, amesema kuwa maandalizi ya kumbukumbu ya kifo cha hayati Edward Moringe Sokoine yamekamilika kwa asilimia 100 huku wanaridha nao zaidi ya elfu moja nao wakithibitisha kumuenzi kwa kukimbia.
Magesa aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati akiongelea maandalizi ya kumbukumbu hizo zinazotarajiwa kufanyika nyumbani kwa hayati Sokoine kesho.
Aidha, alidai kuwa wanariadha zaidi ya 1,000 wamethibitisha kushiriki mbio za kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani Edward Moringe Sokoine zitakazo fanyika wilayani Monduli.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya  Mrisho Kikwete.
Mulongo alisema kuwa wao kama viongozi wa serikali wanaamini kuwa kwa kuandaa michezo mbalimbali ni njia mojawapo ya kukumbuka jinsi ambavyo kiongozi huyo alivyokuwa anapenda na kuthamini michezo.
Lakini pia alisema kuwa mbali na kuweza kuweka utaratibu wa michezo lakini pia maazimisho hayo yatakwenda pamoja na maonesho ya vyuo vikuu.
"Mpaka sasa vyuo vikuu viwili vimeshathibitisha ushiriki wao katika siku hiyo ambayo itakwenda na mambo mbalimbali na hivi vyuo vitatukumbusha tulikotoka kwa miaka hiyo 30 iliyopita," aliongeza Mulongo.
Maazimisho hayo yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali kama vile Rais Kikwete, Mama Maria Nyerere, Rais mstaafu Benjamin Mkapa, pamoja na viongozi wengine kutoka Zanzibar, viongozi wa mashirika ya umma na binafsi, pamoja na wananchi wa Mkoa wa Arusha.

No comments:

Zilizosomwa zaidi