
Aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Robert Semtutu na wenzake wanne,
wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka mawili
yakiwamo ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. milioni 200.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni
aliyekuwa Afisa Ugavi wa Tanesco, Hanin Mahambo, Mkurugenzi wa Fedha,
Lusekeo Kasanga, Mwanasheria Godson Ezekiel na Mkandarasi Martin
Abraham.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Isdore Kyando alidai kuwa
washtakiwa walifanya makosa hayo katika tarehe tofauti mwaka 2011.
Kyando alidai kuwa katika shitaka la
kwanza, Desemba, mwaka 2011 katika ofisi za Tanesco Ubungo jijini Dar es
Salaam washtakiwa walitumia madaraka yao vibaya kwa kufanikisha malipo
kwa msambazaji M/S Young Dong Electronic Co Ltd bila kuhakikisha
Mkandarasi anafika katika kituo cha mwisho.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment