Timu ya Wigan imeichapa Man City
magoli 2-1 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Etihad katika hatua
ya robo fainali ya kombe la FA.
Jodri Gomez aliindikia Wigan goli la
kwanza kwa mkwaju wa penati mnamo dakika ya 27, wakati James Perch
alipachika goli la pili katika dakika ya 34 na kuiwezesha timu hiyo
kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 mpaka timu hizo zikienda mapumziko,
Samir Nasri alipiga msumari wa moto na kumwacha mlinda mlango wa Wigan
akishangaa na kuiwezesha timu hiyo kulipa goli 1 lakini mpaka mwisho wa
mchezo, Man City ilijikuta ikiondolewa katika mtanange huonkwa jumla ya
magoli 2-1.
Matokeo ya mchezo huo yameifanya timu
ya Man City kutolewa katika kinyang'anyiro cha kombe hilo, itakumbukwa
kuwa Man City walitolewa na Wigan katika fainali za kombe la FA mwaka
jana, hivyo kichapo cha leo ni pigo jingine kwa timu hiyo ambayo siku
chache zijazo itakumbana na Barcelona katika mchezo wa raundi ya pili ya
kombe la klabu bingwa ya ulaya.
No comments:
Post a Comment