
Mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua iliyoanza
kunyesha muda wa asubuhi, pia yalisababisha hasara kubwa kutokana na
vitu na mali mbalimbali kusombwa na maji.
Barabara kadhaa zilikuwa hazipitiki kutokana na
kujaa maji, huku baadhi ya nguzo za umeme na simu ambazo zilikuwa karibu
na mifereji ziliharibiwa na kusombwa na maji.
Athari kubwa ya mafuriko hayo ilitokea katika eneo la Kigogo
Darajani ambako baadhi ya nyumba zilikuwa zimejaa maji na baadhi ya vitu
vilionekana vikielea kwenye mikondo mikubwa ya maji.
Mmoja wa waathirika hao, Andrew Simon (35) alisema
nyumba yake ilijaa maji kwa takriban futi nne kwenda juu na kusababisha
hasara ya mali ambayo alikuwa bado hajafahamu thamani yake.
No comments:
Post a Comment