Wanachama
wa Chama cha Mapinduzi wakisherehekea ushindi jioni hii katika ofisi
kuu ya CCM mkoa wa Iringa ambapo inaonyesha CCM wanaongoza kwa mbali
katika matokeo ya awali kwenye uchaguzi wa mbunge wa jimbo la Kalenga
uliofanyika leo mkoni Iringa watu wengi walijitokeza asubuhi kupiga kura
na hali ilikuwa ni ya utulivu kabisa watu wengi waliopiga kura
wameishukuru serikali na tume ya uchaguzi kwa kuandaa utaratibu mzuri na
kufanyika kwa uchaguzi wenye utulivu. mpaka sasa matokeo hayo
yanaonyesha CCM inaongoza kata sita kati ya kata kumi na tatu za jimbo
hilo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-LAKENGA)
Wana CCM wakiendelea kuserebuka kwa muziki kama wanavyoonekana.
No comments:
Post a Comment