Sunday, October 13, 2013

HII NI HABARI KAMILI YA KUPIGWA RISASI MWANDISHI WA HABARI UFOO SARO

Mtangazaji wa ITV anayejulikana kwa  jina  la  Ufoo Saro  amejeruhiwa  vibaya  kwa  kupigwa  risasi  na  mchumba  wake ambaye pia alimuu na mama mkwe wake kisha naye alijipiga risasi na kujiua Alfajiri  ya  leo.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kamanda Wambura  amethibitisha tukio hilo alipoongea na Radio One nakusema kuwa Ufoo alipigwa risasi na mchumba wake ambae anafanya kazi  katika umoja wa mataifa ( UN ) huko Sudani ila bado haijafahamika  kitengo alichokuwa  akifanyia  kazi.


Habari zinasema kuwa mchumba wake huyo alirudi jana nchini Tanzania na kufikia nyumbani kwa Ufoo. Hivyo kulitokea ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe)kibamba kupata suluhu.

Walipofika kwa Mama Ufoo na kuanza kikao cha kutafuta suluhu ndipo ilipoonekana kuwa mwanaume ndio tatizo. Kutokana na hali hiyo, mwanaume alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa  na  mazoea  ya  kumtetea mwanae, kwa hasira akatoa bastola na kumpiga mama mkwe wake kichwani na kumuua papo hapo.

Baada ya kumpiga Mama Ufoo na kumuua  ndipo alipomgeukia Ufoo Saro na kumpiga nae risasi mbili, moja ya tumboni na nyingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia papo hapo.

Kwa taarifa zilizopatikana kuwa, Ufoo Saro anaendelea vizuri akiwa amelazwa ICU  akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.
 Ufoo Saro baada ya kufanyiwa upasuaji huo.
 Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akimpeleka wodini Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro,  baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa risasi kufuatia kushambuliwa kwa silaha ya moto nyumbani kwa mama yake  Kibamba jijini Dar es Salaam leo na mtu aliyedaiwa kuwa ni mchumba wake ambaye pia alimuua mama yake na kisha kujiua.
 Wanahabari wakimpiga picha Ufoo Saro baada ya kuondolewa chumba cha upasuaji.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsindikiza Ufoo Saro wakati akipelekwa wodini.
 

No comments:

Zilizosomwa zaidi