Friday, September 27, 2013

WIKI YA NENDA KWA USALAMA YAFIKIA KILELE LEO HUKO JIJINI MWANZA

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge amefunga wiki ya kwenda kwa usalama leo hii Jijini Mwanza baada ya kufunguliwa mwanzoni mwa wiki hii na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge, akitoa hotuba ya kufunga Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani leo yaliyokuwa yakiadhimishwa Kitaifa katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima, kulia ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge (watatu kushoto) kutoa hotuba ya kufunga Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyokuwa yakiadhimishwa Kitaifa katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Washiriki wa maonesho, wananchi mbalimbali wakiingia ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba kwa maandamano ya kufunga maadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani leo. Maadhimisho ya Nenda kwa Usalama yamefungwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Maneja Masoko wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Elisante Maleko akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge (wapili kushoto) ya jinsi ya shirika hilo linavyotoa bima za magari, mali, maisha na afya wakati alipokuwa analitembelea banda la shirika hilo katika maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kabla ya kuyafunga maonesho hayo yaliyokuwa yanafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama wa Barabarani, Pereira Ame Silima. Kulia ni Afisa Bima wa shirika hilo Hollo Kazi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Mazingira kutoka Makao Makuu ya Wakala wa Barabarani Tanzania (Tanroads), Zafarani Madayi akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge (wapili kushoto) jinsi Tanroads inavyoweza kutengeneza barabara bora na zenye alama za usalama kwa lengo la kuondoa ajali mbalimbali zinazoweza kutoa barabarani kabla ya kuyafunga maonesho hayo yaliyokuwa yanafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, DCP Mohamed Mpinga, akikionesha kitabu cha taaluma ya ufundishaji wa madereva kilichozinduliwa na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge, kabla ya kufunga maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yaliyokuwa yanafanyika jijini Mwanza. Kulia (waliokaa) ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mkurugenzi wa Radio One, Deogratius Rweyunga (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima, baada ya kupokea cheti cha kuthamini mchango wa Radio hiyo iliyopo Dar es Salaam kwa kutangaza habari mbalimbali za usalama barabarani.  Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yamefungwa rasmi na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge, jijini Mwanza leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments: