Jopo la watalaam u wa Wilaya ya Dodoma, litachunguza
mabaki ya udongo wa jengo la Msikiti wa Manyema, uliongua mwishoni mwa
wiki ili kujiridhisha na hali ya usalama wa vyumba vilivyonusurika na
kujua kama vinafaa kwa matumizi.
Hayo yalisemwa jana na Katibu Tawala wa Wilaya ya
Dodoma, Stephen Humba, alipokuwa akizungumza na gazeti hili, kuhusu
tukio hilo.
Wanaounda jopo hilo ambalo ni utekelezaji wa agizo
la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi, mhandisi wa wilaya,
Kikosi cha Zimamoto, polisi, ofisa wa Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) na Idara ya Afya.
Humba alisema jopo hilo lilitembelea eneo la tukio
Ijumaa iliyopita na kugundua kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya
umeme.
“Walikubalina kuwa wachukue mabaki ya udongo
katika jeno hilo kwa ajili ya kwenda kuupima katika maabara ili kuona
kama jengo hilo litafaa kukarabatiwa ama la,”alisema.
Moto huo ulitokea Ijumaa iliyopita na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na jengo hilo.
Dk. Nchimbi alimuagiza Humba kuunda jopo la
wataalam ili kuchunguza kama vyumba vilivyobaki vinaweza kutumiwa na
waumini ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa binadamu.
No comments:
Post a Comment