Kesi dhidi ya naibu rais wa Kenya William Ruto imeanza kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC , Hague Uholanzi.
Bwana Ruto na Rais Uhuru Kenyatta pamoja na
mwandishi wa habari Joshua Arap Sang, wanatuhumiwa kwa kuhusika na
ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 - madai ambayo wanayakanusha.
Bwana Ruto anayetuhumiwa kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi
mkuu mwaka 2007, alikana mashtaka yote dhidi yake. Vile vile mshtakiwa
mwenza mtangazaji wa redio Joshua Arap Sang pia alikana mashtaka.
Rais Uhuru Kenyatta ambaye pia anatuhumiwa kuhusika na ghasia hizo anatarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo mwezi Novemba.
Majaji wa mahakama hiyo wameelezea
kuwa kesi hizo mbili huenda zikafanyika nyakati tofauti katika kipindi
cha wiki nne kila mmoja, wala sio kwa wakati mmoja kama ilivyokuwa
imepangwa awali .
Hii ni kutokana na ombi la rais Kenyatta kuwa
washukiwa hao hawapaswi kuwa nje ya nchi kwa wakati mmoja kwani kutakuwa
na pengo la uongozi.
Duru zinasema kuwa hii bila shaka ndiyo kesi yenye utata mkubwa zaidi kuwahi kusikilizwa katika historia ya mahakama ya ICC.
Kesi ya Kenyatta inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi Novemba.
Ghasia hizo ambazo zilizuka baada ya aliyekuwa
Waziri Mkuu Raila Odinga kupinga ushindi wa Rais Mstaafu Mwai Kibaki,
zilisababisha vifo vya watu 1,300.
Kisacha kesi za washukiwa wa Kenya kufika Hague
Baadaye Ruto na Kenyatta waliunda muungano walioutumia kugombea uongozi kwenye uchaguzi wa Machi mwaka 2013
Kesi dhidi ya Rais Kenyatta itaanza Novemba 10
Mkataba wa amani uliosaidia kumalizika kwa
ghasia hizo, pia ulipendekeza kuwa wale waliohusika na ghasia
wachukuliwe hatua za kisheria.
Tume iliyoongozwa na jaji Waki ambayo ilikuwa na
jukumu la kuchunguza ghasia hizo, ilipendekeza kuwa ikiwa juhudi za
kuunda mahakama ambayo ingesikiliza kesi hizo Kenya zingefaulu, basi
kesi hizo kesi zisingepelekwe Hague.
Ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007-2008
Bwana Ruto ni afisa wa kwanza mkuu serikalini kufika mbele ya mahakama hiyo.
Mshukiwa mwingine Joshua arap Sang, pia
ameshtakiwa kwa kuchochea ghasia na kusaidia katika kupanga mashambulizi
dhidi ya kabila hasimu.
Mashtaka dhidi ya watatu hoa, Ruto, Kenyatta na Sang yanatokana na ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Mnamo siku ya Alhamisi, bunge la Kenya lilitoa
wito wa Kenya kujiondoa kwenye mahakama hiyo ya kimataifa . Bunge
lilikubali kujadili hoja hiyo.
Mahakama ilisema kuwa kesi zitaendelea, hata ikiwa Kenya itajiondoa kwenye mkataba wa Roma uliounda mahakama ya ICC
Aidha mahakama ya ICC ilianzishwa mwaka 2002 ili kusikiliza kesi za kimataifa za mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu.
No comments:
Post a Comment