Wabunge wa bunge la wawakilishi Nigeria wamerushiana
ngumi wakati wa vikao vya Jumanne baada ya kuzuka bungeni sintofahamu
kuhusu mrengo wa wabunge waliojitenga na chama tawala.
Taarifa hizi ni
kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.
Kituo kimoja cha kibinafsi cha televisheni,
pamoja na vituo vingine vilionyesha picha za mbunge mwanamke akimtosa
kidole usoni kwa ghadhabu mbunge mwenzake wakati mbunge mwanamume
akionekana akichukua kiti nusura kumgonga mwenzake wakati wabunge wengine walionekana wakipigana ngumi.
Mgogoro inasemekana ulianza baada ya mwenyekiti
wa mrengo wa wabunge waliojiondoa kutoka kwa chama tawala, Kawu Baraje,
kuingia bungeni akiandamana na magavana wanaomuunga mkono.
Inaarifiwa spika wa bunge la waakilishi ,Aminu
Tambuwal, aliambia wabunge kuwa Baraje aliomba ruhusa kuwahutubia
wabunge wa mrengo wake kabla ya bunge kuanza vikao vyake.
Lakini kuwepo kwa wabunge hao bungeni
kuliwaghadhibisha mno wafuasi wa chama tawala, PDP,kiasi cha kuzuka
sokomoko bungeni kati ya pande hizo mbili na kumlazimisha bwana Baraje
kukatiza hotuba yake kutokana na kelele bungeni.
Chama tawala PDP kina wabunge wengi zaidi bungeni wakiwa 23 kati ya wabunge wote 36
Aidha chama hicho kimetawala Nigeria tangu
kupata uhuru mwaka 1999 lakini hivi kribuni kimezongwa na migogoro ya
ndani ya chama pamoja na kukabiliwa na upizani wenye ushawishi.
Wananchi wanajiandaa kwa uchaguzi mwaka 2015,
lakini wadadisi wana wasiwai ikiwa chama tawala kitakuwa kimesuluhisha
migogoro yake, huku kikikabiliwa na upinzani mkali.
Mgogoro huu umekuwa ukitokota kwa miezi kadhaa
huku baadhi ya wabunge wakitofautiana kuhusu ikiwa Rais Goodluck
Jonathan aidhinishwe na chama kugombea urais kwa mara nyingine wakati
kuna wanasiasa wengine wanaotaka kugombea urais.
Hii ni mara ya kwanza kwa wabunge wa Nigeria kurushiana ngumi bungeni.
No comments:
Post a Comment