Michoro ya picha ya kwenye paketi za sigara ambayo
inatoa onyo kali dhidi ya kuvuta sigara na kuonyesha madhara ya uvutaji
sigara, hupuuzwa na vijana. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa
nchini Uingereza.
Uingereza ilianza kutumia picha hizo ambazo
zinaonyesha mapafu ambayo yemeathirika kutokana na moshi wa sigara
pamoja na upasuaji wa moyo, mnamo mwaka 2008.
Lakini utafiti huo uliowahusisha
watoto 2,800, uligundua kuwa picha hizo hazikuwazuia vijana wenye kati
ya umri wa miaka 11 hadi 16 kununua na kuvuta sigara.
Hata hivyo, picha hizo ziligeuza maoni ya watu wasiovuta sigara na waraibu wa sigara.
Utafiti uliochapishwa katika jarida la kudhibiti
matumizi ya Tumbaku ulidurusu data kutoka kwa utafiti uliofanyiwa
vijana kuhusu utumizi wa sigara kabla na baada ya picha hizo kuanza
kutumika kwenye paketi za sigara.
Kati ya watoto 2,800 waliohojiwa, mmoja kati ya
watoto kumi alikuwa mvutaji wa sigara, wakati wengine walikuwa hawavuti
sigara na wengine wakiwa wale waliowahi kujaribu kuvuta sigara.
Wakati idadi ya vijana waliofikiria kuwa onyo
hizo zinaweza kuwazuia kuvuta sigara baada ya kuanza kutumiwa , miongoni
mwao wale wanaovuta na wale wasio vuta, idadi ya wale waliojizuia
kuvuta sigara kutokana na onyo za picha hizo ilipanda kwa asilimia moja
kutoka kwa asilimia 13 hadi 14.
Mtafiti mkuu Daktari Crawford Moodie, alisema
kuwa wakati jambo hili linaudhi kwamba picha zilizo kwenye paketi za
sigara haziwezi kuwazuia vijana kuvuta sigara, idadi ndogo ya wale
wanaotii onyo hizi sio mbaya sana.
Lakini pia alisema kulikuwa na tisho la watu
kupuuza kabisa picha hizo na matamshi yanayoonya vikali dhidi ya uvutaji
sigara, kwani picha hizo hazijabadilishwa tangu mwaka 2003 na 2008
mtawalia..
"nchi zengine hubadilisha picha na onyo dhidi ya
uvutaji sigara mara kwa mara na baadhi wanahisi kuwa Uingereza inapaswa
kuzibadilisha.
BBC
No comments:
Post a Comment