Jana usiku majira ya saa moja ilitokea ajali mbaya iliyohusisha
gari aina ya Escudo yenye nambari za
usajili T600 AUC na Coaster yenye nambari za usajili T598 BNS. Ajali hiyo
iliyotokea eneo la Makumira, wilayani Arumeru, jijini Arusha. Kwa mujibu wa
mashuhuda wa ajali hiyo wanasema chanzo cha ajali hiyo wamesema kuwa ni gari
aina ya coaster iliyokua ikitokea jijini Arusha na ilipofika eneo la makumira
ilitaka kupita gari iliyokuwa mbele lakini kabla gari hiyo haijamaliza kuipita
gari hiyo, kumbe mbele kulikua kuna gari aina ya Escudo iliyokua ikitokea Moshi
kuelekea Arusha ndipo zilipokutana uso kwa uso na kusababisha ajali mbaya.
Katika ajali hiyo hakuna hata mtu mmoja
aliyefariki ila dereva wa gari aina ya Escudo aliyefahamika kwa jina moja la
Hussein maarufu kama Baunsa ndie aliyeumia sehemu
za miguuni na kichwani lakini wasamaria wema waliweza kumtoa katika eneo la
ajali na kumuwahisha hospitali.
Hii ndio coaster iliyopata ajali ambayo baada ya ajali ilihama barabarani na kuelekea vichakani.
Huu
ni upande wa mbele wa garri aina ya Suzuki Escudo ambao unaonekana
kuumia sana, na baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wakishangaa jinsi
ambavyo gari hiyo imeharibika.
Huu ndio upande wa mbele wa coaster iliyopata ajali na abiria wote kutoka wakiwa wazima wa afya.
No comments:
Post a Comment