Katika hali ya kawaida mcheza soka akiwa kama mtu maarufu anatazamwa
kama kioo cha jamii ambacho umma hutazama na kufuata tabia nzuri
inayofaa mbele za watu .
Dhana hiyo inaonekana haijaeleweka vyema kwa nyota wa timu ya taifa
ya England na klabu ya Tottenham Hotspurs Kyle Walker ambaye amepigwa
picha inayoonyesha akivuta dawa ya kulevya aina ‘Hippy Crack’.Hippy Crack ni dawa ya kulevya inayovutwa ambayo matumizi yake yameruhusiwa lakini ina madhara yale yale kama dawa nyingine za kulevya kama bangi na kadhalika.
Hippy Crack humlevya mtumiaji na kumfanya awe katika hali ya ‘kurelax’ wakati kilevi chake kikiwa kimekolea.
Walker alikuwa akivuta ‘Mjani’ huo unaowekwa kwenye chombo maalum wakati akiwa kwenye klabu ya usiku siku ya jumamosi ikiwa ni saa 24 baada ya mchezo wa kufuzu kombe la dunia ambao England ilishinda 4-0 dhidi ya Moldova .
Kyle ameomba radhi kwa kitendo hicho ambapo amekiri kosa na anaelewa madhara ya tabia yake akiahidi kutojirudia kwa tukio kama hilo .
Kwa upande mwingine chama cha soka cha England kimeamua kutompa adhabu yoyote mchezaji huyo zaidi ya onyo kwa tukio kama hilo litakalojitokeza siku za baadae.
No comments:
Post a Comment