Manchester United wamefanikiwa kukamilisha usajili wa kiungo Marouane Fellaini akitokea Everton kwa uhamisho wa £27.5million, ikiwa ni masaa machaache tu kabla ya dirisha la usajili kufungwa hapo jana saa 23:59 usiku.
Usajili wa kiungo huyu raia wa Ubelgiji ndio unaonekana kuwa mkubwa kufanywa na David Moyes toka ateuliwe kuwa boss wa Manchester United mara baada ya kuwakosa baadhi ya nyota alionuwia kuwasajili wakiwemo Thiago Alcantara aliyetimkia Bayern Munich, Cesc Fabregas akisalia katika timu yake ya Barcelona.
Pia mapema ilisemekana Manchester United wangemsajili kiungo mchezeshaji kutoka club ya Athletic Bilbao Andre Herrera kwa ada ya uhamisho ya €36million,lakini usajili wake ulishindikana masaa machache kabla ya dirisha la usajili kufungwa hapo jana baada ya mazungumzo yao kutofikiwa muafaka, na hatimaye Manchester United wakaelekeza nguvu zao kwa kuhakikisha wanamsajii Marouane Fellaini.
Hatimaye kiungo huyu wa kimataifa kutoka Ubelgiji ameungana tena na meneja wake wa zamani David Moyes.
Mligo G.
No comments:
Post a Comment