Tuesday, September 3, 2013

UJENZI WA BOMBA LA GESI KUHAMISHA MAKABURI YA KINONDONI..


Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) limetangaza kuhamisha makaburi 37 katika Manispaa ya Kinondoni ili kupisha ujenzi wa bomba jipya la gesi asilia kutoa Songosongo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Yona Kilagane, alieleza hayo juzi katika taarifa yake kwa umma kupitia vyombo vya habari akiwataka wananchi watakaoguswa kuwasiliana na ofisi ya shirika hilo ili kupata utaratibu wa kuyahamisha makaburi hayo.

Aliyataja maeneo yatakayohusika na idadi ya makaburi kwenye mabano kuwa ni Kimara Mavurunza (20) ya Wakristo na Mtaa wa Mbezi Juu, ambapo makaburi 17 ya ukoo wa Mkwawa yataguswa.
Katika taarifa hiyo, ndugu na jamaa wa marehemu hao wametakiwa kufika ofisi za TPDC katika kipindi cha mwezi mmoja ili kupewa utaratibu wa kuhamisha makaburi hayo.

Chanzo T/daima

No comments:

Zilizosomwa zaidi