Mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Kipwa mwambao mwa Ziwa
Tanganyika wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa mwenye miaka minane
ameweza kujiokoa yeye na mtoto wa dada yake mwenye umri wa miezi mitano
kwa kuogelea hadi ufukweni baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama
kwenye ziwa Tanganyika.
Manusura huyo aliyefahamika kwa jina moja la Prisca akiwa miongoni
mwa wengine 15 walinusurika kufa maji ama kwa kuogelea au kuokolewa
alipoona mtumbwi huo ukizama, inadaiwa alipiga mbizi majini akiwa na
mtoto huyo mchanga mgongoni mwake na kuweza kuogelea kwa saa kadhaa hadi
ufukweni wote wakiwa hai.
Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Kipwa katika mwambao wa Ziwa
Tanganyika , Benson Silinjile alithibitisha mkasa huo wa aina yake
akisema msichana huyo Prisca alikuwa amempeleka mtoto huyo kupata chanjo
katika kituo cha afya kijijini Kapele kwa kuwa mama wa mtoto huyo
alikuwa mgonjwa hivyo alimwomba msaada huo.
Licha ya msichana huyo kuweza kujiokoa yeye na mtoto huyo mchanga kwa
kuogelea hadi ufukweni pia nahodha wa mtumbwi huo uliopata ajali hiyo
iliyosababisa vifo vya watu 13 wakiwemo wanawake na watoto wenye umri
chini ya miaka mitano , Lazaro Sikapote (26) aliweza kuokoa familia yake
akiwemo mama yake mzazi Rose Sikapote , mkewe Rakadia Sikazwe na mwanae
aliyefahamika kama Nazaro Sikapote.
Chanzo: Habari leo
No comments:
Post a Comment