Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim
Poulsen ameita kambini wachezaji 24 kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya
Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini
humo.
Wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 mwaka huu kabla
ya saa 1 kamili usiku. Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itakuwa kwenye hoteli ya Accommondia jijini
Dar es Salaam.
Makipa walioitwa katika timu hiyo Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali
(Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Aggrey
Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Nadir
Haroub (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na
David Luhende (Yanga).
Viungo Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu
Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo
(Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga),
John Boko (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo)
na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).
No comments:
Post a Comment