Saturday, August 10, 2013

MECHI YA BARCELONA YABADILISHIWA UWANJA…

Barcelona wakiwa mazoezini
Waandaji wa mechi nchini Malaysia wamelazimika kubadili uwanja utakaotumika kwenye mechi ya kirafiki kati ya Barcelona dhidi ya Malaysia XI kutokana na hali mbaya ya uwanja wa Bukit Jalil National Stadium. 
Uongozi wa mabingwa hao wa La Liga umekubaliana na waandaji wa mechi hiyo ijumaa iliyopita kuwa mchezo huo utapigwa leo usiku dhidi ya Malaysia XI kutokana na kile kinachodaiwa kuwa na hali mbaya ya nyasi katika uwanja wa taifa wa Bukit Jalil.
Sasa mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Shah Alam wenye uwezo wa kuchukua watazamaji  69,000 uliopo nje kidogo ya jiji la Kuala Lumpur, ambao ulifanyiwa mazoezi na Barcelona punde walipowasili Alhamisi iliyopita.
Waziri wa vijana na michezo nchini Malaysia  Khairy Jamaluddin amesema alikwisha tanabaisha hali hiyo mbaya ya nyasi katika uwanja huo na kuamulu uwanja ufungwe kuanzia mwezi Octoba kwa ajili ya kupisha ukarabati.
Pia waziri huyo aliandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa kitendo hicho kimeitia aibu nchi kutokana na usumbufu kwa watu ambao walikwisha nunua tiketi za mchezo huo.
By Mligo G

No comments:

Zilizosomwa zaidi