(Rais wa FA Greg Dyke) |
Mwezi mmoja baada ya rais wa FIFA Sepp Blatter kuahidi kushughulikia mabadiliko ya kombe la dunia 2022 inayotarajiwa kufanyika nchini Qatar, hatimaye rais wa chama cha soka nhini Uingereza (FA) Greg Dyke amemuunga mkono Blatter na kukubali michuano hiyo ya kombe la dunia ifanyike kipindi cha majira ya baridi badala kipindi cha majira ya joto kutokana na joto kuwa kali zaidi.
Mwezi uliopita Blatter alithibitisha kulipeleka suala hilo kwenye bodi ya wakurugenzi ya FIFA kushughulikia mabadiliko hayo. Dyke amesema "huwezi kucheza michuano ya mpira wa miguu nchini Qatar kipindi cha mwezi wa sita.
No comments:
Post a Comment