|
Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hudson amemuonya
mshambuliaji wa Mancheter United Wyne Rooney kuwa kunahatari ya yeye kupoteza
nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa endopo hatapata nafasi ya kupangwa
kikosi cha kwanza katika club yake.
Rooney amekuwa akihofia nafasi yake ya kucheza katika kikosi
cha kwanza cha Man United kutokana na meneja mpya wa mabingwa hao wa England
David Moyes kumpa kipaumbele mshambuliaji Robin Van Persie, huku mabingwa hao
wameshakataa ofa mbili kutoka kwa wapinzani wao Chelsea kutaka kumsajili
Rooney.
Wyne Rooney |
Hudson amesema itakua ngumu sana kuendelea kumchagua mchezaji
wa miaka 27 kama hapati nafasi kucheza mara kwa mara kwenye club yake.
Jina la Rooney limetajwa kwenye kikosi cha England
kinachojiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Scotland itakayopigwa katika
uwanja wa Wembley Jumatano ingawa ameikosa micheza yote ya kabla ya msimu
ambayo Man United imecheza kwenye tua yao huko Asia kutokana na majeraha
aliyoyapata mwanzoni mwa tua hiyo ya Man United.
By Mligo G
No comments:
Post a Comment