Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) ushirika wa Segerea limenusurika kuteketea kwa
moto baada ya watu wasiojulikana kutupa chupa iliyodhaniwa kuwa na
mafuta ya taa au ya petroli na kulipuka ndani ya kanisa na kuunguza
baadhi ya vitu vilivyowemo katika madhabahu ya kanisa pamoja na gari
lililokuwa nje ya kanisa hilo majira ya saa 8 usiku
wa kuamkia jana.
Akielezea
tukio hilo mchungaji wa kanisa la KKKT usharika wa Segerea Bwana Noha
Kipingu, amesema tukio limetokea majira ya saa 8 za usiku
,wakati baadhi ya waumini wakiwa ndani ya kanisa katika maombezi ya
yaliyoanza saa 4 usiku kwa ajili ya mkutano uliokuwa unaotarajiwa kufanyika
jumapili ya leo agosti 25.
Akielezea
msimamo wa kanisa KKKT usharika wa Segerea kuhusu tukio hilo, licha ya
kusisitiza linachukuliwa kama sehemu ya matukio mengine ya ulipuaji wa
makanisa yanayoendelea,amesema kwa mujibu wa maelezo ya mlinzi wa kanisa
ameona watu wanne waliotega chupa na kulipua kwenye gari la kanisa
pamoja na kurusha chupa nyingine ndani na kisha kukimbia.
Baadhi
ya waumini walionusurika katika tukio hilo wamesema wamesikia mshindo
mkubwa wa kitu kinachofanana na bomu katika madhabau ya kanisa hilo
wakati wakiwa wamesimama mbele ya kanisa hilo na kisha moto ukaanza
kuunguza madhabau hali iliyowafanya kukimbia na kisha kurudi ndani kwa
ajili ya kuzima moto huo.
No comments:
Post a Comment