Mpaka sasa watu watatu wamepatikana
wakiwa wamefariki
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es
salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea
mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29,
2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili
wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa
mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye
kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa
ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe saidi
Meck Sadiki katika eneo la jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi
jijini Dar es salaam asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013
ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili
wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa
mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye
kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa
ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
No comments:
Post a Comment