Mkuu
wa polisi mkoani Rift Valley John M'mbijiwe anayedaiwa kuwa na uhusiano
na mtu huyo mlaghai,John Waiganjo ingawa alikana kumfahamu
Maafisa watatu waandamizi wa
polisi nchini Kenya, wamesimamishwa kazi kuhusiana na sakata ya mtu
mmoja ambaye aliwalaghai watu kuwa yeye ni naibu kamishna mkuu wa polisi
kwa zaidi ya miaka mitano.
Mkuu wa polisi mkoani Rift Valley John M'mbijiwe
anayedaiwa kuwa na uhusiano na mtu huyo mlaghai,John Waiganjo ingawa
alikana kumfahamu ni mmoja wa wale waliofutwa kazi.Wiki iliyopita, Joshua Waiganjo, alifikishwa mahakamani, kwa kujifanya afisa mwandamizi wa polisi katika mkoa wa Rift Valley.
Mshukiwa huyo amekanusha madai hayo.
Ripoti zinasema kuwa ulaghai huo ulifichuliwa, wakati aliposafiri kwa ndege ya polisi, kwenda kuchunguza mauaji wa maafisa 42 wa polisi waliouawa na wezi wa ng'ombe katika bonde la Suguta, tukio ambalo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya taifa hilo.
Bwana Kavulundi amesema kuwa mkuu wa polisi
mkoani humo John M'Mbijiwe, afisa mkuu wa kitengo cha polisi cha
kupambana na wezi wa mifugo ASTU Remi Ngugi na afisa mkuu wa polisi
wilayani Njoro Peter Nthiga wamesimamishwa kazi.
Amesema watatu hao huenda wakahujumu uchunguzi ikiwa wataendelea kusalia madarakani.
Joshua Waiganjo amesemekana kuwafuta kazi na kuwaajiri maafisa wengine wa polisi katika mkoa wa Rift Valley wakati huo.
Baada ya kukana mashtaka hayo, kesi hiyo ilihairishwa ili kumruhusu mshukiwa huyo kutafuta matibabu kutokana na ugonjwa wa kisukari katika hospitali moja nchini humo.
KUTOKA BBC

No comments:
Post a Comment