Monday, January 14, 2013

MAMIA WAZUNGUMZIA SUALA LA GESI KUTOKA MTWARA...


Wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi nchini Tanzania waendelea na malalamiko yao dhidi ya mpango wa serikali kujenga bomba la kusafirisha gesi iliyogunduliwa katika mikoa hiyo ya kusini na kusafirishwa hadi Dar es Salaam.

Wakuu wa usalama walivunja mpango wa maandamano na mkutano ulopangwa wa wanafunzi wa vyuo vya Iringa siku ya Jumapili Januari 13, 2012. Wanafunzi wanaopinga mpango huo wa serikali unaozusha utata, wanadai kwamba sehemu kubwa ya rasilmali hiyo inabidi kuwanufaisha wakazi wa mikoa hiyo badala ya kusafirishwa nje.

Mapema mwezi wa Januari wabunge kutoka Mkoa wa Mtwara waliwalaumu wakuu wa mikoa hiyo ya Mtwara na Lindi kwa kutowaelimisha wananchi juu ya mpango huo baada ya kupelekwa nchi za nje kupata maarifa juu ya namna ya kuwahamasisha wananchi kuhusiana na masuala hayo ya uzalishaji gesi na mafuta.

Mhadhiri wa masuala ya kiuchumi katika chuo kikuu cha Mzumbe, Bakari Mohamed, anasema inabidi kuhakikisha kwamba mapato ya gesi yanabidi kuwanufaisha kwanza wakazi wa mikoa hiyo katika Nyanja zote kabla ya maslahi mengine yoyote ile.

Onesmo Olenguruma, mwanasheria na mtetezi wa haki za binadam anasema kutokana na hictoria ya Tanzania wananchi wa Mtwara na Lindi wanahaki ya kutetea maslahi yao kufuatana na katiba na hasa kutokana na historia ya nchi juu ya namna inavyo tumia rasilmali zake.

Anasema kawaida wananchi wa maeneo ambako rasilmali asili inapatikana hawafaidiki na utajiri huo, kutokana na hiyo inabidi kuwepo na sera na mipango kabambe ya serikali za kuwashirikisha na hapo huwenda wakaridhika
.
Wakati huo huo wakazi wa mikoa mingine ya Tanzania wameanza kuunga mkono madai ya wakazi wa Mtwara na Lindi kudhibiti sehemu kubwa ya mapato ya gesi inayopatikana huko kusini mwa Tanzania

No comments:

Zilizosomwa zaidi