Wednesday, January 16, 2013

HII NDIO STORI KAMILI KUHUSU OKWI KUCHEZEA SOKA TUNISIA

BAADA ya kuhangaika muda mrefu hatimaye mshambuliaji wa mabingwa wa Tanzania Bara, Simba na timu ya taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi amejiunga naklabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa gharama ya Ddola 300,000 (sawa na Sshs 477 milioni).
Okwi alisaini mkataba huo wa kuichezea timu hiyo kwamuda miaka mitatu na nusu mbele ya Mmwenyekiti wa Simba,Ismail Aden Rage na Rrais wa Etoile, Ridha Charfeddinejana Jumanne mchana Okwi ambaye mwishoni mwa mwaka jana aliongeza mkataba wa kuichezea Simba mpaka mwaka 2014, ameuzwa kwa dola za kimarekani 300,000, na kuweka rekodi ya mauzo yajuu kwa klabu hiyo.Katika mkataba huo Okwi aneweka kibindoni dola100,000 kwa kukubali kusaini mkataba huo pamoja nakulipwa mshahara wa Ddola 15,000 kwa mwezi.
Habari hiyo iliyothibitishwa na OAfisa Habari wa klabu hiyo,Ezekiel Kamwaga zilisema kuwa Simbailiwakilishwa namwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage kukamilishazoezi hilo.

Okwi aliyekuwa katika majaribio na timu hiyo uhamishowake ulifanyika harakaa haraka ili kuwahi mwisho wa usajiliwa nchi hiyo.Mchezaji huyo wa Uganda, mara kadhaa amekuwa gumzokatika usajili na katika dirisha dogo, liliwalazimu viongozi waSimba kumfuata Uganda na kumsainisha kwa miaka miwili.

Hatua hiyo ilitokana na uvumi kuwa mchezaji huyo alikuwana mpango wa kujiunga na watani wa jadi wa Simba, Yangana klabu ya Azam FC ambazo zilidaiwa kutoa ofa kubwakwa mchezaji huyo.Katika usajili wa mwanzoni mwa mwaka jana, Okwi alikimbiliakusaka timu nje ya nchi, hata hivyo pamoja na kufanya vizuri,hakuweza kucheza huko na kurejea katika timu yake yaSimba.

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwagaalisema kuwa ni kweli kuwa Okwi ameuzwa kwa timu hiyo,hata hivyo hakuwa tayari kuweka bayana masuala mbalimbali ya mkataba wa mchezaji huyo.“Nipo likizo, taarifa hizo ni za kweli, lakini kutokana na haliilivyo, mwenyekiti wa timu, Rage atakuja kuelezea kwa kinasuala la mchezaji huyo na kuhusiana na marlupurlupu menginepamoja na makubaliano hasa mshahara, kwa sasa sinataarifa zaidi ya kuuzwa kwa mchezaji huyo,” alisemaKamwaga. Alisema kuwa anajua kuwa Okwi hakwenda na timu Omankwa ajili ya mazoezi ya maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu yaTanzania Bara na michuano ya kimataifa na vile vile anajuataarifa za kuondoka kwa Rage kwenda huko kukamilishazoezi la mauzo ya mchezaji huyo.

Miaka miwili iliyopita, Simba iliuzwa wachezaji wake wawili,Mbwana Samatta and Mganda Patrick Ochan kwa klabuya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa Ddola 100,000 (Sshs150 milioni ) kila mmoja.Kutokana na kuuzwa kwa Okwi, Simba sasa inabakiwa na
wachezaji wanne wa kigeni, Mzambia Felix Sunzu, KomabilKeita (Mali), Mussa Mudde na kipa Abel Dhaira kutoka Uganda.

No comments:

Zilizosomwa zaidi