CHAMA cha
Soka mkoa wa Kagera (KRFA), kimempinga Rais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Leodegar Tenga na kamati yake ya utendaji kwa kupinga
mchakato wa marekebisho ya Katiba ya shirikisho hilo.
Mwenyekiti
wa KRFA, Jamali Malinzi amesema kuwa katika kikao cha kamati yake ya
utendaji kilichoketi Desemba Mosi mjini Bukoba wamekubaliana kutoshiriki
mchakato wa marekebisho hayo ya katiba yanayoendeshwa kwa njia ya
waraka na kudai kuwa ni batili.
"Mchakato
wa TFF wa kubadili katiba ya TFF kama ulivyoanishwa katika warakata wa
TFF kwa vyama wanachama wake ni batili kwa kuwa haukidhi matakwa ya
katiba ya TFF kifungu cha 22 (1).
Kifungu hicho cha 22 kinasema kuwa mkutano mkuu wa TFF ndio pekee wenye
mamlaka ya kubadili katiba ya TFF, aidha kifungu kidogo cha 30 1-6
kinaeleza taratibu nzima ya mchakato wa kubadili katiba ikiwa ni pamoja
na kutoa notisi ya siku 45, kuitisha mkutano mkuu na kupigak ura na
wajumbe theluthi mbili kuridhia.
"Hakuna
mahali popote kwenye katiba ya TFF panapotamka kuwa katiba ya TFF
itabadilishwa kwa wanachama kuzungushiwa waraka kupiga kura na kuandika
jina na saini na kisha kuituma kura makao makuu ya TFF sisi kama KRFA
hatutashiriki.
"alisisitiza
Malinzi
Mapema wiki hii Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisikika akisistiza kuwa
mchakato huo wa kubadili Katiba ya TFF kwa njia ya waraka uendelee
kufanyika kwasababu shirikisho hilo hivi sasa halina pesa za kuitisha
mkutano mkuu kwa ajili ya zoezi hilo na kuwataka wanachama wake
kukubaliana na njia hiyo.
"Tunataka
katiba yetu ilindwe na iheshimiwe na watu wote mana katiba ndio
muongozo mkuu wa vipi mpira uendeshwe nchini mwetu, Katiba ya TFF ndio
iliyomuweka Tenga madarakani pamoja na kamati yake ya utendaji, katiba
inatutawala wote hakuna aliye juu ya katiba.
" alisema
Malinzi alionyesha kushangazwa na kauli ya TFF kudai kuwa ufinyu wa
bajeti kuwa ni kikwanzo kikuu kinachozuia mkutano mkuu wa kubadili
katiba usifanyike.
"TFF bila kujali kama vyama vya mikoa vina pesa au la ilitoa ratiba ya
chaguzi za mikoa na kusisitiza ifuatwe, TFF haikutoa hata shilingi moja
kusaidia zoezi hili, iweje wao washindwe kama mikoa inayojiendesha bila
vyanzo vyovyote vya mapato iliweza sababu hii haina matinki.
"alisema
kwa kuhoji
Alisema TFF inatakiwa kuitisha mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba ya
shirikisho hilo kwa faida ya soka la Tanzania ikiwa ni pamoja na
kuepukana na marumbano mbalimbli yanayoweza kujitokeza endapo litakiuka
taratibu.
Katika
hatua nyingine, Malinzi alisema kitendo cha kuwambia kipengele cha club
licencing kisipoingizwa kwenye katiba ya TFF basi vilabu vya Simba na
Azam vitazuiwa kushiriki michuano ya CAF mwakani ni kichekesho kwa kuwa
TFF taarifa ya kutakiwa kuingizwa kipengele hicho walikuwa nazo mapema
toka mwaka 2006 kwenye mkutano wa Fifa uliofanyika Berlin, Ujerumani
mwaka huo na kusainiwa na Rais wa Fifa Sepp Blatter Oktoba 29 mwaka 2007
na agizo hilo lilisisitizwa iwapo kipengele hicho hakitaingizwa klabu
hazitaruhusiwa kushiriki michuano ya CAF na Fifa.
"Tenga
ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya CAF baada ya kupokea waraka wa FIFA
kuhusu suala hili alikaa na kutoa ratiba ya mchakato wa utekelezaji wa
agizo hilo, ratiba ilionyesha hadi Desemba 2011 kila nchi mwanachama wa
CAF ilitakiwa iwe imeingiza, siku saba zimesalia tangu amalize muda wake
wa uongozi Desemba 14 tunambiwa Simba na Azam tusipotisha kipengele
hiki hazitashiriki.
"Mwezi
April mwaka huu TFF ilifanya mkutano wake mbona hawakukiweka kipengele
hiki kama ajenda?"alihoji na kusema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha
4.5.1. kwenye waraka wa FIFA kinaruhusu nchi wanachama kuombea kibali
klabu zake na kuitaka TFF kufanya hivyo kwa kuziombea kibali cha
kushiriki michuano ya CAF mwakani timu za Simba na Azam.
No comments:
Post a Comment